• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michezoni: Wada yaweza kuipa adhabu mpya Russia kwa kushindwa kuwasilisha data

  (GMT+08:00) 2019-01-02 09:06:06

  Russia inaweza kukabiliwa na adhabu mpya ya kufungiwa kwenye michezo baada ya Shirika la Kupambana na Dawa za Kusisimua misuli (Wada) jana kuthibitisha kuwa nchi hiyo imeshindwa kuwasilisha data hadi kufikia tarehe ya mwisho ambayo ni December 31 kutoka maabara yake ya kukabiliana na dawa za kusisimua misuli ya Moscow. Rais wa Wada Craig Reedie amesema amesikitishwa kwamba zoezi la kuchukua data kwenye maabara ya zamani ya Moscow halikukamilika kwa wakati hadi tarehe ya mwisho waliyokubaliana. Wada imesema Kamati huru ya Utekelezaji wa Ukaguzi (CRC) sasa itafikiria hatua nyingine katika mkutano wa Januari 14 na15.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako