• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania:Uchumi unaweza kuathirika iwapo wafadhili hawatatoa misaada

  (GMT+08:00) 2019-01-02 19:47:05

  Shirika la Kimataifa la kutathmini Mikopo la FITCH Ratings limeonya kuwa ukuaji wa uchumi haraka wa Tanzania huenda ukaathiriwa iwapo serikali itatia doa mahusiano yake na baadhi ya washirika wakuu wa maendeleo wa nchi hiyo,ikiwemo Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya.

  Wakati Tanzania inatarajiwa kurekodi ukuaji mkbuwa wa pato la Taifa barani Afrika mwaka 2019 na zaidi,tishio la usistishaji wa misaada,na ucheleweshwaji katika utekelezaji wa miradi mikuu ya miundombinu kama ule wa gesi asilia mkoani Lindi,huenda ukaathiri matarajio ya ukuaji wa uchumi wa nchi hiyo.

  Katika Ripoti yake,Shirika la Fitch linasema kuwa Tanzania inaweza kuharibu mahusiano yake na washirika wakuu wa maendeleo ikiwemo Benki ya Dunia na Umoja wa Ulaya kutokana na sera za serikali.

  Shirika la FITCH aidha linasema kuwa mikopo kutoka mashirika makuu kama vile Benki ya Dunia ni vyanzo muhimu vya fedha za kigeni kwa Tanzania na hufadhili miradi mingi ya maendeleo katika sekta za uchukuzi,elimu,maji na sekta nyenginezo.

  Hivi karibuni Waziri wa Fedha na Mipango wa Tanzania Dkt Philip Mpango alikiri kuwa nchi inapitia wakati mgumu kutokana na uamuzi wa baadhi ya washirika wa maendeleo kusitisha msaada kwa serikali.

  Hata hivyo Waziri huyo wakati akizindua Ripoti ya Hali ya Uchumi jijini Dodoma,alisema Tanzania haitateteleka katika msimamo na uhuru wake kwa kutii shinikizo kutoka magharibi za kutaka kupitishwa kwa haki za mashoga nchini humo ili kupata misaada.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako