• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kundi la kwanza la mabasi ya mwendokasi kuwasili Kenya kutoka Afrika Kusini mwezi huu

  (GMT+08:00) 2019-01-02 19:47:22

  Waziri wa uchukuzi nchini Kenya James Macharia amesema kuwa serikali imeagiza mabasi 64 ya mwendo kasi kutoka Afrika Kusini.

  Wiki iliyopita Waziri macharia alisema serikali inapanga kununua mabasi hayo kuitoka Afrika Kusini kwa sababu watengenazaji mabasi wa ndani wameshindwa kufikia viwango vinavyohitajika.

  Mabasi hayo yatahudumu katika barabara kuu ya Thika na barabara nyengine kuu ndani ya jiji kuu la Nairobi.

  Hata hivyo Waziri Macharia alisema wananunua mabasi hayo ya mwanzo kutoka Afrika Kusini,lakini mengine yataagizwa nchini.

  Hatua hiyo imewakera wazalishaji wa ndani ambao wanadai kuwa wana uwezo wa kuunda mabasi hayo.

  Mabasi hayo yanatarajiwa kuwasili nchini kutoka Afrika Kusini mwezi huu.

  Serikali itazindua barabara tano za mabasi hayo ya BRT jijini Nairobi katika hatua inayolenga kupunguza msongamano wa magari jijini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako