• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Waziri asisitiza umuhimu wa kudumisha mabaraza ya Biashara

    (GMT+08:00) 2019-01-02 19:47:37

    Ni mikoa 11 tu Tanzania ambayo imefanikiwa kudumisha mabaraza ya biashara ambayo yalianzishwa nchini humo.

    Haya yalibainishwa na Waziri wa Taifa katika Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera,Bunge,Ajira,Vijana na Wasiojiweza) ,Jenista Mhagama alipokuwa ziarani katika mkoa wa Kigoma.

    Alisema mikoa hiyo ni pamoja na Dodoma,Kigoma,Tanga,Geita,Morogoro,Shinyanga,Dar es Salaam,Pwani,Iringa,Songwe na Mbeya.

    Mhagama alionya kuwa mikoa ambayo mabaraza yake ya biashara hayajakuwa yakifanya kazi yanaenda kinyume na agizo la Rais nambari 1 la mwaka 2001,ambalo linaagiza kubuniwa na kudumisha mabaraza hayo.

    Alisisitiza kuwa mabaraza hayo ni muhimu katika kuhakikisha kuwa biashara zinafanikiwa katika ngazi za mitaa.

    Waziri Mhagama alisema kuwa mabaraza yote ya mikoa na wilaya yalilengwa kuwa vyombo vya kuunda mifumo ya serikali na sekta binafsi ya kujadili masuala ya uboreshaji wa biashara na mazingira ya uwekezaji katika ngazi zilizolengwa.

    Alisema pia mabaraza hayo ynafaa kutumiwa kama vyombo vya kukuza na kutangaza fursa za biashara zinazopatikana katika serikali zote za mitaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako