• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaitaka Marekani kushughulikia suala linalohusiana na Taiwan kwa tahadhari

    (GMT+08:00) 2019-01-02 19:54:58

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, suala la Taiwan ni mambo ya ndani ya kisiasa ya China, ambalo linahusiana na maslahi makuu ya China na hisia ya taifa la China na haliwezi kuingiliwa na nguvu ya nje. China inaitaka Marekani kufuata kanuni ya China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani na kushughulikia suala linalohusiana na Taiwan kwa tahadhari.

    Habari zinasema, hivi karibuni muswada wa pendekezo la kutoa tena uhakikisho kwa Asia mwaka 2018 umepitishwa. Muswada huo ni pamoja na kuimarisha mawasiliano ya kiserikali na uhusiano wa kijeshi kati ya Marekani na Taiwan, lakini hauna nguvu ya kisheria.

    Bw. Lu amesema, muswada huo umekiuka kanuni ya Kuwepo kwa China moja na taarifa tatu za pamoja za China na Marekani, ambao pia umeingilia vibaya mambo ya ndani ya China. China inapinga vikali kupitishwa kwa muswada huo kwa Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako