• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Emery atetea uamuzi wake wa kumtoa uwanjani, Alexandre Lacazette

  (GMT+08:00) 2019-01-03 09:18:06

  Meneja wa Arsenal, Unai Emery, ametetea uamuzi wake wa kumtoa uwanjani, Alexandre Lacazette wakati wa mechi yao dhidi ya Fulham ambayo walishinda magoli 4-1 juzi. Kiungo huyo mshambuliaji kutoka Ufaransa aliwafungia washika bunduki hao goli la pili kwenye kipindi cha pili kwenye dakika ya 55, lakini, aliondolewa uwanjani na nafasi yake ikachukuliwa na raia wa Wales, Aaron Ramsey. Wakati huo, Arsenal ilikuwa mbele kwa 2-1 baada ya Aboubakar Kamara kuifungia Fulham kwenye dakika ya 69. Uamuzi wa kutolewa Lacazette ulikosolewa na mashabiki wengi katika uwanja wa Emirates. Lakini, Ramsey alilipa imani ya Emery kwa kufunga bao katika dakika ya 79 kabla ya Aubameyang kukamilisha ushindi wao katika dakika ya 83.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako