• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michezo Mingine: Nado yaitaka Wada kuichukulia hatua haraka Russia

  (GMT+08:00) 2019-01-03 09:19:49

  Mashirika ya taifa ya kupambana na dawa za kusisimua misuli Nado yamesema, Shirika la Kupambana na dawa za kusisimua misuli Duniani linapaswa kuchukua hatua haraka dhidi ya Russia kwa kushindwa kufikia tarehe ya mwisho kuwasilisha data za wanamichezo wake kutoka maabara yake ya kukabiliana na dawa za kusisimua misuli ya Moscow. Rais wa Wada Craig Reedie ambaye anakalia kiti moto, juzi alitangaza kwamba amesikitishwa sana na Russia kwa kutofikia tarehe ya mwisho, na kupanga kufanya mkutano wa Kamati huru ya Utekelezaji wa Ukaguzi (CRC) Januari 14 na15. Lakini kwenye taarifa yao ya pamoja viongozi wa Nado wamesema ni lazima mkutano ufanyike mapema na nchi hiyo ichukuliwe hatua haraka. Mwezi Septemba Wada iliiondolea marufuku Shirika la Kupambana na Dawa za kusisimua Misuli la Russian (Rusada), na kuwapa nafasi wanariadha wa nchi hiyo kurejea kwenye mashindano ya michezo mbalimbali, uamuzi ambao umeibua hisia kali dhidi ya Wada hasa kwa rais wa Wada Reedie.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako