• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uganda: Kampuni ya China yawasilisha ombi la kujenga barabara ya Jinja-Kampala

  (GMT+08:00) 2019-01-03 19:44:04

  Kampuni ya ujenzi ya China Railway imewasilisha ombi la kujenga barabara kuu kati ya mji wa Jinja na Kampala nchini Uganda.

  Ujumbe wa maafisa wa kampuni hiyo ukiongozwa na mwenyekiti wake wa maswala ya biashara ya Afrika bwana He Ping umekutana na Rais Museveni ili kujadili uwezekano wa kupata kandarasi hiyo.

  Bwana Ping amsema iwapo watapewa kandarasi wangependa kushirikiana na mkandarasi wa Uagnda ili kujenga barabara hiyo ya urefu wa kilomita 95.

  Mji wa Jinja uliopo mashariki mwa Uganda unavutia watalii wengi kwani ndio chanzo cha mto Nile kwenye ziwa la Victoria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako