• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Ada mpya za kusafirisha mizigo kwa SGR zaahirishwa hadi Machi

  (GMT+08:00) 2019-01-03 19:46:52

  Waagizaji ambao walinunua bidhaa kabla ya Desemba 31 hawatalipa ongezeko la ushuru la asilimia 79.

  Serikali ilikuwa imetangaza ongezeko la ushuru kwa bidhaa zote zinazosafisishwa kupitia kwa reli ya kisasa SGR kutoka mjini Mombasa hadi mji mkuu Nairobi.

  Waagizaji wamepewa mpaka mwishoni mwa mwezi Machi kusafirisha bidhaa zao kwa bei iliopunguzwa kupitia SGR.

  Hata hivyo Chama cha Wafanyabiashara wa Kenya (KAM) kimeombea kuendelea kuchelewesha kwa viwango vipya, wakisema vitaongeza gharama ya kufanya biashara.

  Gharama ya kusafirisha kontena la futi 20 kutoka Mombasa hadi Nairobi iliongezeka Jumanne hadi dola 500 kutoka dola 350.

  Nayo kontena ya futi 40 inasafirishwa kwa dola 700 kutoka dola 400 za awali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako