• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: Ggodi wa kampuni ya Gem and Rock Venture waagizwa kuanza kazi mara moja

  (GMT+08:00) 2019-01-03 19:47:10

  Naibu Waziri wa Madini, wa Tanzania Dotto Biteko, ameagiza mgodi wa kampuni ya Gem and Rock Venture, uliokuwa na mgogoro wa mpaka na kampuni ya Tanzanite One tangu Julai mwaka jana, uanze kazi mara moja.

  Aliyasema hayo alipotembelea migodi ya madini ya tanzanite mji mdogo wa Mirerani, wilayani Simanjiro.

  Alisema mgogoro wa kampuni ya TanzaniteOne na Gem and Rock Venture unatakiwa kumalizika na kampuni hiyo iendeshe shughuli zake za uchimbaji wa madini.

  Mgogoro wa kugombea mpaka wa chini mgodini kwa kampuni hizo ni wa muda mrefu na umeasababisha kampuni hiyo isimamishwe kufanya kazi tangu mwaka jana.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako