• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tenisi: Tanzania kuandaa mashindano ya tenisi kwa vijana Afrika, "Tennis Zonal Championship"

    (GMT+08:00) 2019-01-04 09:04:01

    Mashindano ya tenisi kwa vijana Afrika, Tennis Zonal Championship, yanatarajiwa kufanyika kuanzia Januari 7 hadi 15, 2019, viwanja wa Gymkhana, jijini Dare es Salaam, yakishirikisha jumla ya nchi 10. Rais wa chama cha tenisi Tanzania TTA, Denis Makoi amesema nchi zitakazo shiriki ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Comoro, Sudan, Somalia, Ethiopia, Eritrea, Ushelisheli, pamoja na Tanzania kama mwenyeji. Aidha amesema TTA kwa kushirikiana na shirikisho la mchezo wa Tenisi Afrika (CAT) na shirikisho la Tenisi Duniani (ITF) wamejipanga vyema kuhakikisha mashindano hayo yanafanikiwa na timu bora kushinda, huku mazingira mazuri yameandaliwa kwa timu hizo kupata malazi mazuri kipindi chote cha mashindano. Mashindano hayo yatahusisha vijana kati ya umri wa miaka 14 na 16, na washindi watapata tiketi ya kushiriki mashindano ya tenisi ya Afrika mwezi Aprili mwaka huu, katika nchi za Afrika Kusini na Morocco.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako