• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: Kocha wa Manchester United aweka rekodi iliyowekwa tangu mwaka 1946

    (GMT+08:00) 2019-01-04 09:04:49

    Kocha wa Manchester United Mnorway ameweka rekodi ya zaidi ya miaka 70 ambayo haikuwekwa kwa muda mrefu katika klabu ya Manchester United. Baada ya ushindi wa juzi dhidi ya Newcastle unaifanya Manchester United kushinda michezo minne mfululizo baada ya kupata kocha mpya. Mshambuliaji Mbelgiji Romelu Lukaku aliingia kama mchezaji wa ziada yaani superSub na kufunga goli baada ya kugusa mpira kwa mara yake ya kwanza baada ya kuingia uwanjani na kuiwezesha Manchester United kuwalaza Newcastle United kwa 2-0. Rashford aliongeza bao la pili dakika ya 80. Baada ya ushindi huo sasa raia huyo wa Norway ameifikia rekodi ya meneja maarufu Sir Matt Busby aliyefanya hivyo mwaka 1946, kwa kushinda michezo minne mfululizo akiwa kama kocha mpya aliyekabidhiwa timu. Baada ya ushindi wa kuridhisha dhidi ya Cardiff, Huddersfield na Bournemouth, mechi hiyo ya Jumatano ilikuwa mtihani mkubwa zaidi kwa Manchester United chini ya Solskjaer.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako