• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Soka: CAF latangaza waamuzi watakaochezesha mechi ya Simba na JS Saoura

    (GMT+08:00) 2019-01-04 09:05:05

    Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limetangaza waamuzi watakaochezesha mechi ya Klabu Bingwa Afrika kati ya Simba na JS Saoura. Waamuzi hao ni Joshua Bondo ambaye atasimama kama mwamuzi wa kati, waamuzi wasaidizi Oamogetse Godisamang, Moemedi Godfrey Monakwane na mwamuzi wa akiba, Kutlwano Leso, wote kutoka nchini Botswana.

    Kamishna wa mechi ni James Leonard Mwenda kutoka nchini Malawi, msimamizi mkuu wa mchezo huo ni Alexander Sakyi Asante kutoka nchini Ghana. Simba itawakaribisha JS Saoura katika mchezo huo wa kwanza wa hatua ya makundi ambao utapigwa Januari 12 Jijini Dar es salaam. Ikumbukwe Simba ipo katika kundi D pamoja na vigogo wawili ambao ni Al Ahly ya Misri na AS Vita Club ya Congo DRC pamoja na JS Saoura ya Algeria ambayo haina uzoefu mkubwa katika michuano hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako