• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Soka: Liverpool yakubali kupoteza mbele ya Manchester City

  (GMT+08:00) 2019-01-04 09:06:33

  Liverpool imekubali kupoteza mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia leo dhidi ya Manchester City kwa kufungwa mabao 2-1. Mabao ya City yamewekwa kimiani na Sergio Kun Arguero na Leroy Sane huku Liverpool ikifuta machozi kupitia kwa Roberto Firmino. Ushindi huo wa Manchester City unakuwa wa kwanza baada ya mechi tano mfululizo katika EPL kushindwa kupata matokeo mbele ya Liverpool. Kupoteza kwa Liverpool kumeifanya ikubali kufungwa mabao mawili msimu huu EPL ndani ya mechi moja na ikipoteza mchezo wa kwanza. Msimamo unaonesha hivi sasa Liverpool bado ipo kileleni ikiwa na pointi 54 kwa tofauti ya alama 4 na Man City iliyo na 50.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako