• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uwanja wa Mao Tse Tung uliojengwa na kampuni ya China wazinduliwa rasmi visiwani Zanzibar

    (GMT+08:00) 2019-01-04 09:06:57

    Uwanja wa michezo wa Mao Tse Tung uliopo eneo la Maisara visiwani Unguja ambao umejengwa na kampuni kutoka China umezinduliwa rasmi jioni ya jana Alhamisi huku serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ikichangia Sh 4 bilioni. Viwanja hivyo viwili vina uwezo wa kubeba mashabiki 1,200 waliosimama na waliokaa jukwaani 900. Uwanja huo pia una maeneo mengi ya kuchezea michezo ya ndani kama uwanja wa mazoezi ya viungo (gym), mpira wa kikapu, netboli na mingineyo. Imeelezwa mbele ya Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr Ali Mohamed Shein kuwa uwanja huo umejengwa ndani ya miaka mitano na kampuni kutoka China ambao wametengeneza viwanja viwili. Imefafanuliwa kuwa ujenzi huo ni msaada wa Wachina, lakini serikali ilitoa fedha hizo kwa ajili ya majengo ya ofisi zilizomo ndani ya uwanja huo, ukuta na viwanja vya michezo mingine.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako