• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kriketi: Kocha wa Kriketi U-19 wa Kenya asema ana muda mfupi kujiandaa na kombe la dunia

  (GMT+08:00) 2019-01-04 09:07:18

  Kocha wa timu ya Kriketi ya vijana chini ya miaka 19 ya Kenya, Jimmy Kamande, ana chini ya miezi mitatu kukusanya kikosi chake kitakachoshindana kwenye michuano ya Afrika ya kufuzu kombe la Dunia Division One iliyoandaliwa na Shirikisho la Kimataifa la Kriketi (ICC) ambayo itafanyika Windhoek, Namibia kuanzia Machi 15 hadi 24. Kamande amesema ilimchukua miaka miwili kuandaa kikosi kilichofuzu michuano ya mwaka jana ya kombe la dunia. Lakini safari hii bado hajachagua kikosi chake kutoka na mpango huo kuvurugika vibaya na kusita Juni mwaka jana kutokana na migongano ya kiuongozi. Hata hivyo amesisitiza kuwa atachagua wachezaji chini ya miaka 16 ambapo kama hawakufuzu kwenye kombe la dunia la 2020, wataweza kupata uzoefu utakaowasaidia kwenye mashindano ya kufuzu ya mwaka 2022 yatakayofanyika West Indies. Timu sita zikiwemo Kenya, Uganda, Tanzania, Nigeria, Sierra Leone na wenyeji Namibia zitapambana kuwania kucheza Kombe la Dunia kwa vijana chini ya miaka 19 litakalochezwa 2020 huko Afrika Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako