• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima wa Ukambani Kenya wakata tama na kungoa mikahawa yao

    (GMT+08:00) 2019-01-04 20:53:17

    Mwaka uliopita wa 2018, wakulima wa zao la kahawa janibu za ukambani walikabiliwa na changamoto na masaibu chungu nzima, nusra wakate tamaa na kuweka chini zana zao za ukulima kwa kukosa matumaini.

    Hali ilikuwa mbaya kiasi kwamba baadhi yao waliamua kung'oa mikahawa yao na kukumbatia kilimo mbadala cha mboga na matunda ili waweze angalau kukidhi mahitaji yao ya kimsingi, kando na kugharamia karo za watoto wao.

    Kwa mfano, kati ya mwaka wa 2015 na 2016 bei ya kilo moja ya kahawa ilikuwa Sh75 kwa kilo. Lakini kuanzia mwanzoni mwa mwaka wa 2017 bei hiyo ilishuka hadi Sh28 kwa kilo moja ya kahawa ghafi. Hii ina maana kuwa mkulima ambaye aliwasilisha kilo 10,000 ya kahawa kiwandani kwa mwaka angetia kibindoni takriban Sh750,000, kabla ya kuondoa gharama za uzalishaji.

    Lakini sasa kiasi hicho cha mapato kimepungua hadi kufikia Sh280,000 ambapo baada ya kutoa gharama za pembejeo za kilimo na ujira wa vibarua, mapato hayo yatasalia finyu mno.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako