• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wakulima walaumu kamati kwa kuchelewa kuwasilisha ripoti

    (GMT+08:00) 2019-01-04 20:53:38

    Wakulima na viongozi wa eneo la North Rift wameilaumu kamati iliyoteuliwa kuchunguza kashfa ya mahindi kwa kutowasilisha ripoti yao kwa rais Uhuru Kenyatta kabla ya mwaka mpya ndipo wajue hatma yao kabla ya shule kufunguliwa.

    Wakulima hao waliozugumza na Radio China Kimataifa wamewakashfu Magavana wa Uasin Gishu na Trans-Nzoia kwa kuchelewa kuikabili Serikali kuyanunua mahindi kwa bei ya juu ikizingatiwa kuwa gharama ya kuyakuza iko juu.

    Wakulima hao waliyasema hayo baada ya rais Kenyatta kusema kuwa hajapokea ripoti ya mahindi licha ya tangazo kutoka kwa gavana wa Uasin Gishu Bw Jackson Mandago, Desemba 20, 2018 kwamba ripoti hiyo itapelekewa Rais Desemba 24, 2018. Wakulima wengi wamechanganyikiwa kwa sababu wanayategemea mahindi kulipia watoto wao karo za shule.Shule tayari zimefungunguliwa na maghala ya kuhifadhi mahindi ya halmashauri ya nafaka na mazao (NCPB) bado hayajafunguliwa. Kucheleweshwa kufunguliwa kwa maghala haya kunamaanisha wakulima watakabiliwa na wakati mgumu kulipa karo za shule.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako