• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Simba SC yatinga nusu fainali

  (GMT+08:00) 2019-01-07 08:55:59
  Michezo kadhaa imeendelea mwishoni mwa wikiendi, ikishuhudiwa Azam fc ikiichapa Yanga mabao 3-0 katika hatua ya makundi. Magoli ya Azam yalifungwa na Obrey Chirwa aliyegusa nyavu za Yanga mara mbili na goli la tatu lilifungwa na Ennock Atta.

  Mechi nyingine ilipigwa jana kati ya Simba SC na KMKM, bao pekee la chipukizi Rashid Juma limeipa Simba ushindi wa 1-0 katika mchezo huo wa kundi A jana usiku uwanja wa Amani.

  Kikosi cha kwanza cha Simba kinarejea jijini Dar es salaam leo kujiandaa na michuano nya klabu bingwa Afrika dhidi ya JS Saouara ya Algeria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako