• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mchakato wa kumtangaza Harden kuwa mchezaji bora wa wakati wote wa NBA

  (GMT+08:00) 2019-01-07 08:56:23
  Mkurugenzi wa timu ya Houston Rockets inayoshiriki ligi ya kikapu nchini Marekani Daryl Morey amesema ipo haja ya kumtangaza mchezaji wa timu yake hiyo James Harden kuwa mchezaji mahiri wa mchezo wa mpira wa kikapu wa chama cha mchezo huo nchini humo NBA.

  Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Morey amesema Harden anastahili kutokana mafanikio aliyoyapata katika mechi mfululizo alizoshiriki katika cha miaka kumi hadi hivi leo, kwani amefanikiwa kupata takwimu binafsi za umahiri zilizo bora kuliko mchezaji mwingine katika ligi hiyo.

  Kwa msimu huu pekee, Harden ana wastani wa alama 33.6 za ufungaji, na 15 za usaidizi, na katika mechi ya mwisho iliyofanyika mwishoni mwa juma lililopita alikuwa chachu ya ushindi wa alama 134-135 dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi Golden State Warriors.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako