• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kampuni ya ufaransa kujenga megawati 40 Eldoret

    (GMT+08:00) 2019-01-07 18:44:51

    Kampuni ya Ufaransa ya kutengeneza umeme wa jua Alten Afrika imetangaza kushirikiana na kampuni ya kutengeneza kawi endelevu ya Voltalia kutengeneza megawati 40 za umeme mjini Eldoret. Alten imesema Voltalia tayari ilianza ujenzi huo katika kaunti ya Uasin Gishu Disemba mwaka jana.Alten Afrika ilitoa idhini kwa Voltalia kuanza ujenzi huo.Kiwanda hicho ambacho kipo katika kaunti ya Uasin Gishu kwenye hekari 100 tayari kimeweka paneli elfu 161 kunasa jua kwa ajili ya kutengeneza umeme. Pia Alten imefahamisha kampuni ya kitaifa ya kusambaza umeme KPLC kuhusu mradi huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako