Rais wa chama cha tenisi Tanzania TTA, Denis Makoi amesema nchi zinazozishiriki ni Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Comoro, Sudan, Somalia, Ethiopia, Eritrea, Ushelisheli, pamoja na mwenyeji Tanzania.
Aidha amesema TTA kwa kushirikiana na shirikisho la mchezo wa Tenisi Afrika (CAT) na shirikisho la Tenisi Duniani (ITF) wamejipanga vyema katika kuhakikisha mashindano hayo yanafanikiwa na timu bora kushinda, huku mazingira mazuri yameandaliwa kwa timu hizo kupata malazi mazuri kipindi chote cha mashindano.
Mashindano hayo yatahusisha vijana wa umri wa miaka 14 na 16, na washindi watapata tiketi ya kushiriki mashindano ya tenisi ya Afrika mwezi Aprili mwaka huu, katika nchi za Afrika Kusini na Morocco.
© China Radio International.CRI. All Rights Reserved. 16A Shijingshan Road, Beijing, China. 100040 |