• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • AFC Leopards Kikaangoni baada ya mashabiki kumcharaza Mwamuzi

  (GMT+08:00) 2019-01-08 09:38:44
  Klabu ya AFC Leopards ya Kenya imetakiwa kuweka hadharani majina ya mashabiki wake waliomwangushia kipigo msimamizi wa mechi kati yao na Nzoia Sugar mchezo uliopigwa jumapili iliyopita kwenye uga wa Kenyatta Machakos.

  Rais wa Shirikisho la soka nchini Kenya (FKF) Nick Mwendwa ameapa kuichukulia hatua kali AFC Leopards ambao pia walikuwa mwenyeji wa mechi hiyo akieleza kuwa vurugu na ukosefu wa maadili katika soka nchini humo ni suala ambalo limepitwa na wakati na halikubaliki kamwe.

  Mashabiki wa Ingwe walijitosa uwanjani baada ya kipenga cha mwisho kupigwa na kuanza kumshambulia mwamuzi huyo wakilalamikia bao la dakika za lala salama lililowekwa kimiani na Nzoia Sugar.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako