• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhalifu wa kutumia silaha na milipuko nchini China wapungua katika mwaka 2018

    (GMT+08:00) 2019-01-08 18:23:23

    Wizara ya Usalama wa Umma nchini China imesema, uhalifu wa kutumia silaha na milipuko nchini humo ulipungua kwa asilimia 27.6 na asilimia 29 mwaka jana ikilinganishwa na mwaka 2017, idadi inayoiweka China kwenye orodha ya nchi zenye uhalifu mdogo wa kutumia silaha na milipuko duniani.

    Msemaji wa wizara hiyo Guo Lin amesema, kuanzia Januari hadi Novemba mwaka jana, kesi 42 za uhalifu wa kutumia silaha na 39 za milipuko zilishuhudiwa nchini China. Katika kipindi hicho, polisi nchini China walishughulikia kesi zaidi ya elfu 37 zinazohusiana na uhalifu wa kutumia silaha na milipuko na kukamata watuhumiwa elfu 43.

    Amesema msako ulioanza mapema mwaka jana ulichukuliwa kama kampeni ya kitaifa, na kufanya hatua hiyo kuwa ya vitendo zaidi na uhakika, na kwamba tangu kuanza kwa kampeni hiyo, mamlaka kote nchini China zilipokea zaidi ya taarifa 500 kutoka kwa umma kuhusiana na uhalifu wa kutumia silaha na vifaa vya milipuko.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako