• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yaunga mkono Korea Kaskazini na Marekani kuendelea kufanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2019-01-08 19:21:28

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo hapa Beijing amesema, China inatumai na kuunga mkono Korea Kaskazini na Marekani kuendelea kufanya mazungumzo, na kupata matokeo mazuri.

    Lu Kang amesema hayo wakati kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong Un yuko ziarani hapa China kuanzia jana hadi Alhamisi wiki hii. Bw. Lu Kang amesema, mawasiliano kati ya viongozi wa China na Korea Kaskazini ni sehemu muhimu ya urafiki wa jadi kati ya nchi hizo mbili, na siku zote China inaona kuwa, mawasiliano kati ya Marekani na Korea Kaskazini yana manufaa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako