• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • China yatoa tuzo kwa wanasayansi waliotoa mchango muhimu

  (GMT+08:00) 2019-01-08 19:35:22

  Mkutano wa kutoa tuzo za sayansi na teknolojia ulioandaliwa na Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China na Baraza la Serikali la China umefanyika leo hapa Beijing. Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi wa chama na serikali akiwemo rais Xi Jinping, pamoja na wanasayansi waliotoa mchango muhimu kwa ajili ya maendeleo ya sayansi na teknolojia nchini China.

  Kwenye mkutano huo, rais Xi Jinping amekabidhi tuzo ya ngazi ya juu zaidi ya sayansi na teknolojia ya mwaka 2018 kwa Bw. Liu Yongtan ambaye ni mwanataaluma wa akademia ya China anayefanya kazi katika Chuo Kikuu cha Viwanda cha Harbin, na Bw. Qian Qihu ambaye pia ni mwanataaluma wa akademia na ni mfanyakazi katika Chuo Kikuu cha Uhandisi cha jeshi la nchi kavu la China. Pia rais Xi ametoa hati pamoja na wanataaluma hao wawili kwa wanasayansi waliopewa tuzo za sayansi ya kimaumbile, uvumbuzi wa teknolojia, na maendeleo ya sayansi na teknolojia, na ushirikiano wa kimataifa katika mambo ya sayansi.

  Bw. Liu Yongtan mwenye umri wa miaka 82 amepewa tuzo kutokana na mafanikio yake ya utafiti wa mfumo wa rada. Anasema,

  "Tumepata mazingira mazuri ya utafiti kutokana na sera ya mageuzi na kufungua mlango. Katika miaka 40 iliyopita, nimenufaika sana na sera hiyo. Niliposoma nje ya nchi, niliamua kutoa mchango kwa ajili ya maendeleo ya taifa ambalo liko nyuma kimaendeleo. Pesa haina maana kwetu, Vitu muhimu zaidi ni malengo na uzalendo."

  Mkutano huo wa mwaka 2018 umetoa tuzo kwa miradi 278 na wanasayansi 7. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya tuzo za sayansi na teknolojia ya China Bw. Chen Zhimin amesema, kati ya miradi iliyopewa tuzo, matokeo ya utafiti wa kimsingi yamejitokeza, na kuongeza ushawishi wa China duniani, wakati huo huo, tuzo hizo pia zimeonesha uungaji mkono wa maendeleo ya sayansi na teknolojia kwa uchumi na maisha ya watu. Anasema,

  "Katika miradi iliyopewa tuzo za mwaka 2018, uvumbuzi wa teknolojia za sekta za uchumi umepiga hatua kubwa, na kuunga mkono maendeleo ya uchumi. Aidha, matokeo ya utafiti wa sayansi na teknolojia kwa ajili ya kuboresha maisha ya watu na mazingira ya kiasili yamepatikana kwa wingi."

  Aidha kampuni za China zimeanza kujitokeza katika jukwaa la tuzo la sayansi na teknolojia. Kati ya miradi 134 iliyopewa tuzo, theluthi moja imefanywa na kampuni hizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako