• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UNHCR yafanya kampeni ya mshikamano na wakimbizi

  (GMT+08:00) 2019-01-09 09:30:42

  Shirika la kuhudumia wakimbizi la Umoja wa Mataifa UNHCR limetangaza kampeni mpya ya kimataifa inayowataka watu duniani kote kutembea umbali wanaosafiri wakimbizi kila mwaka.

  Kampeni hiyo inayoitwa "Safari ya kilomita bilioni 2 kutafuta usalama" inawataka watu washiriki kwa pamoja katika kukimbia, kutembea au kupanda baiskeli ili kufikia jumla ya umbali wa kilomita bilioni mbili. Washiriki wanaweza kutumia programu zao za mazoezi kwenye simu au tovuti ya kampeni hiyo (www. Stepwithrefugees.org), ili kuchangia lengo hilo. Kampeni hiyo itawahimiza watu kusaidia wakimbizi kwa kuimarisha mshikamano.

  UNHCR imesema washiriki wanaweza kutafuta udhamini, kwa lengo la kukusanya dola za kimarekani milioni 15 ili kusaidia na kutoa huduma za usajili na mapokezi, chakula na maji, makazi, msaada wa msingi, huduma za afya na msaada wa kisaikolojia kwa wakimbizi.

  Shirika la Uhamiaji la Umoja wa Mataifa IOM limesema watu zaidi ya 3,000 wamekufa au kupotea wakiwa njiani kwenye uhamiaji kwa mwaka wa tano mfululizo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako