• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tuzo za Mwanasoka bora wa Afrika

    (GMT+08:00) 2019-01-09 09:51:36

    Hatimaye Afrika imefahamu washindi wa tuzo za mwanasoka bora wa bara la Afrika kama ilivyotolewa na Shirikisho la kandanda Afrika (CAF) jana jumanne kwa wanasoka waliofanya vizuri mwaka 2018.

    Hafla ya utoaji tuzo hizo imefanyika jana mjini Dakar Senegal na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa siasa na michezo. Mohamed Salah anayekipiga ligi ya EPL katika klabu ya Liverpool na mchezaji wa taifa wa Misri amenyakua tuzo ya mchezaji bora wa kiume, huku tuzo ya mchezaji bora wa kike imekwenda kwa Chrestinah Thembi Kgatlana wa Afrika Kusini na timu ya Houston Dash. Kwa upande wa mwanasoka bora chipukizi tuzo imechukuliwa na Achraf Hakimi wa Morocco anaykipiga katika klabu ya Dortmund, Kocha bora wa kiume ni Herve Renard wa Morocco huku kocha bora kwa upande wa wanawake ni Desiree Ellis wa Afrika Kusini. Timu bora ya taifa ya wanaume tuzo imekwenda kwa timu ya taifa ya Mauritania, kwa upande wa timu bora ya taifa kwa wanawake tuzo imekwenda kwa timu ya taifa ya wanawake ya Nigeria. Tuzo zingine ni ya heshima amepewa rais wa Senegal Macky Sall, tuzo ya rais bora wa shirikisho la soka imekwenda kwa Fouzi Lekjaa na goli bora la mwaka aliyepata tuzo ni Chrestinah Thembi Kgatlana wa Afrika Kusini anayechezea klabu ya Houston Dash.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako