• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kutoa hatua mpya za kuhimiza matumizi ya wananchi na kupanua kufungua mlango

    (GMT+08:00) 2019-01-09 18:58:31

    Naibu mkurugenzi wa kamati kuu ya maendeleo na mageuzi ya China Bw. Ning Jizhe amesema, ili kuhakikisha uchumi wa China unaendelea kwa kasi inayofaa, China itatoa sera husika katika kuongeza matumizi ya watu na uwekezaji wenye ufanisi na pande nyingine, na itaendelea kupanua maeneo yanayowekezwa na wafanyabiashara wa nchi za nje, na kupanua kufungua mlango.

    Bw. Ning Jizhe amesema, kwa sasa pato la watu wa China limeongezeka, hivyo sera zinapaswa kuendana na mwekeleo wa kuongezeka kwa kiwango cha matumizi ya wananchi, ili kutoa umuhimu wa kimsingi kwa ajili ya maendeleo ya uchumi, ikiwa ni pamoja na kuhimiza manunuzi ya magari na vifaa vya nyumbani.

    Pia amesema, kamati hiyo itafuata agizo lililotolewa kwenye mkutano wa Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China kuhusu kazi za uchumi, ambalo linataka kuhimiza kufungua mlango kwa pande zote na kwa kiwango cha juu, kuboresha mazingira ya kutumia uwekezaji kutoka nje, kuhimiza miradi mikubwa ya uwekezaji kutoka nje kutekelezwa kwa haraka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako