• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania ina upungufu wa tani 260,000 za sukari

    (GMT+08:00) 2019-01-09 20:03:51
    Serikali ya Tanzania imesema kwa sasa taifa linakabiliwa na upungufu wa sukari wa zaidi ya tani 260,000.

    Naibu Waziri wa Kilimo Omary Mgumba amesema kuwa taifa lina upungufu wa tani 155,000 ya sukari ya viwandani na upungufu wa zaidi ya tani 105,000 ya sukari ya matumizi ya nyumbani.

    Mgumba aliyasema hayo jana wakati alipozuru kiwanda cha uzalishaji sukari cha TPC Moshi.

    Aidha Mgumba alisema serikali itahakikisha inamaliza upungufu huo wa sukari,na kuwataka wawekezaji waeleze serikali changamoto wanazokumbana nazo wakati wa uzalishaji ili wakae chini na kutafuta njia bora za kuzitatua.

    Katika ziara hiyo Naibu Waziri Mgumba aliongozana na Mkurugenzi Mkuu wa Bodi ya sukari Tanzania (SBT),Profesa Kenneth Bengesi.

    Akizungumza wakati wa ziara hiyo,Profesa Bengesi alisema kuwa bado mahitaji ya sukari nchini Tanznaia ni makubwa na kuwataka wawekezaji waliowekeza katika viwanda vya sukari kuitazama fursa hiyo na kuifanyia kazi.

    Profesa Bengesi alisema kuwa kutokana na mahitaji hayo wameweka mazingira rafiki ya wawekezaji kuwekeza kuwekeza katika sekta ya sukari.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako