• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya kuwa mwenyeji wa kongamano la kimataifa la zao la macadamia

  (GMT+08:00) 2019-01-09 20:09:54

  Uzalishaji wa kiwango kidogo unaoongezeka wa zao la macadamia nchini Kenya umetambulika duniani na kuifanya Kenya kuwa mwenyeji wa kongamano la tisa la kimataifa la zao la macadamia mwezi Agosti 2021.

  Kongamano hilo,ambalo huandaliwa kila baada ya miaka miwili,huwaleta pamoja wataalamu,wasomi,wajasiriamali na wakulima kutoka pande mablimbali za dunia kujadilia kuhusu mafanikio na kupanga mikakati ya kuendeleza sekta hiyo.

  Afisa Mkuu Mtendaji wa Chama cha usindikaji korosho na macadamia nchini Kenya (NutPAK) Charles Muigai anasema Kenya ilichaguliwa kuwa mwenyeji wa kongamano hilo kutokana na mafanikio ya sekta hiyo.

  Chama hicho ni moja ya waandaaji wakuu,huku kongamano hilo likitarajiwa kuhudhuriwa na wajumbe 800.

  Wazalishaji wengine kama vile China,Afrika Kusini na Australia wana mashamba makubwa ya macadamia.

  Kenya ina takriban mashamba madogo 200,000 yanayokuza macadamia.

  Kulingana na chama cha NutPAK,mashamba hayo kwa sasa yanazalisha tani 42,500,takriban asilimia 20 ya usambazaji wa zao hilo duniani.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako