• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Uchumi wa Afrika Kusini watarajiwa kukua kwa asilimia 1.3 kwa mwaka huu

  (GMT+08:00) 2019-01-10 08:41:30

  Ripoti mpya kuhusu uchumi wa dunia iliyotolewa na Benki ya dunia inasema pato la ndani la taifa GDP la Afrika kusini linakadiriwa kukua kwa asilimia 1.3 mwaka huu, kutokana na vizuizi vya mahitaji ya ndani na matumizi ya serikali.

  Ripoti inasema wakati ukuaji wa uchumi wa Afrika kusini umedorora kwa zaidi ya miaka mitano, makadirio yanaonesha kuwa mwelekeo huo utaendelea katika miaka ijayo, na ukuaji unakadiriwa kuwa asilimia 1.7 na asilimia 1.9 kwa mwaka 2020 na 2021 mtawalia.

  Ripoti pia inaonesha kuwa ukuaji wa uchumi wa nchi za Afrika kusini mwa Sahara unatarajiwa kufikia asilimia 3.4 mwaka huu. Uchumi wa Nigeria na Angola unakadiriwa kuongezeka kwa asilimia 2.2 na asilimia 2.9 mtawalia mwaka huu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako