• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Sudan yapinga taarifa ya nchi za Troika kuhusu maandamano yaliyotokea nchini humo

  (GMT+08:00) 2019-01-10 08:41:50

  Serikali ya Sudan imeeleza kupinga taarifa iliyotolewa na nchi za Troika yaani Uingereza, Norway na Marekani, pamoja na Canada juu ya maandamano yaliyotokea hivi karibuni nchini Sudan.

  Wizara ya mambo ya nje ya Sudan imesema kupitia taarifa kuwa inapinga na kulaani taarifa hiyo isiyo ya haki na inayoenda kinyume na ukweli, ambayo ilitolewa Jumanne na Balozi za Troika na Canada, juu ya maandamano yaliyotokea hivi karibuni kwenye baadhi ya maeneo nchini Sudan na hatua zilizochukuliwa na idara husika kukabiliana na maandamano hayo.

  Serikali ya Sudan imesisitiza dhamira yake ya kulinda uhuru wa kutoa maoni na mikutano ya hadhara ya amani kama ilivyoagizwa na Katiba ya nchi, lakini haihusishi shughuli haramu na za kimabavu zinazolenga kutimiza malengo haramu na kutishia usalama na utulivu wa nchi.

  Jumanne nchi za Troika na Canada zilitoa taarifa zikieleza wasiwasi mkubwa kuhusu hatua zinazochulikuwa na serikali ya Sudan kukabiliana na maandamano yaliyotokea nchini humo, na kuwaweka kizuizini wanaharakati wa kisiaisa na wapinzani bila kufuata utaratibu wa kisheria.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako