• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda yapiga marufuku kupandisha karo ya shule za sekondari na zile zinazosaidiwa na serikali

  (GMT+08:00) 2019-01-10 09:04:15

  Serikali ya Rwanda imetangaza kupiga marufuku kupandishwa kwa karo kwa wanafunzi wanaosoma katika shule za sekondari za umma na zile zinazosaidiwa na serikali, kabla ya kuanza muhula mpya wa masomo. Uamuzi huu umetolewa baada ya wazazi kulalamika kuwa shule zinawataka kutoa fedha zaidi.

  Akiongea jana mjini Kigali, Waziri wa Elimu wa Rwanda Bw Eugene Mutimura amesema wasiwasi umejitokeza kutokana na mzigo wanaotwishwa wazazi, unaoweza kuwazuia wanafunzi kutoka familia maskini kupata elimu.

  Amesema kupanda kwa karo kunaweza kukwamisha juhudi za serikali kutoa elimu kwa wote, na kusema serikali imetoa mwongozo kwa waziri ya serikali za mitaa, kuzitaka wilaya zihakikishe kuwa shule hazipandishi karo kabla ya kuwasiliana na mamlaka za wilaya.

  Wizara ya elimu ya Rwanda imesema kwa sasa kuna shule za umma 460, na shule 871 zinazosaidiwa na serikali.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako