• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yatakiwa kuongeza uzalishaji wa ngano ili kupunguza uagizaji wa chakula - CIMMYT

  (GMT+08:00) 2019-01-10 09:04:37

  Kituo cha kimataifa cha kuboresha uzalishaji wa mahindi na ngano (CIMMYT) kimesema kitahimiza uzalishaji wa ngano nchini Kenya, ili kuisaidia nchi hiyo kupunguza uagizaji wa chakula.

  Mwakilishi wa Afrika kwenye kituo hicho Bw. Stephen Mugo amesema kama ilivyo kwa nchi mbalimbali za Afrika kusini mwa Sahara, Kenya inakabiliwa na ongezeko la mahitaji ya bidhaa za ngano kama mikate, wakati uzalishaji wa ngano umekwama au unapungua.

  Kwa mujibu wa takwimu za serikali, mwaka 2017 Kenya ilizalisha tani laki 1.6, zikiwa zimepungua kutoka tani laki 2.14 za mwaka 2017. Takwimu pia zinaonyesha kuwa mwaka jana Kenya iliagiza tani milioni 1.86.

  Bw. Mugo amesema wakulima wa Kenya wakiwa na njia sahihi za kilimo, wanaweza kuongeza uzalishaji wa ngano kutoka wastani wa tani mbili wa sasa hadi tani sita kwa hekta.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako