• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • UN yasema Yemen inapaswa kufikia maendeleo ya kibinadamu baada ya kusaini Makubaliano ya Stockholm

  (GMT+08:00) 2019-01-10 09:15:17

  Naibu katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia mambo ya kibinadamu Bw Mark Lowcock ametoa wito wa kuwepo kwa maendeleo kwenye masuala ya kibinadamu nchini Yemen, baada ya kutekeleza usimamishaji vita unaoiletea Hodeidah hali ya utulivu.

  Serikali ya Yemen na kundi la waasi la Houthi walikubaliana kusimamisha vita katika mazungumzo yaliyofanyika mjini Stokholm Sweden mwezi uliopita, na Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio namba 2451 na kuidhinisha Makubaliano hayo.

  Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa nchini Yemen Bw Martin Griffiths, amesema serikali ya Yemen na kundi la waasi la Houthi wametekeleza ahadi kuhusu makubaliano ya usimamishaji vita huko Hodeidah, yaliyoanza kutekelezwa tarehe 18 mwezi uliopita, na sasa mapambano kati yao yamepungua. Mjumbe maalum wa China nchini Yemen pia ametoa wito kwa pande zote mbili zitekeleze makubaliano hayo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako