• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Marais wa Afrika Kusini, Zambia watoa mwito wa kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi DRC

  (GMT+08:00) 2019-01-10 09:20:48

  Rais Cyril Ramaphosa wa Afrika Kusini na mwenzake wa Zambia Bw. Edgar Lungu wameitaka tume ya uchaguzi wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo CENI kutangaza matokeo ya uchaguzi wa rais.

  Rais Lungu ambaye pia ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika SADC amefanya ziara ya kikazi nchini Afrika Kusini.

  Msemaji wa idara ya mahusiano ya kimataifa na ushirikiano ya Afrika Kusini Bw. Ndivhuwo Mabaya amesema, marais hao wawili wameitaka CENI kumaliza haraka mahesabu ya kura na kutoa matokeo ya uchaguzi ili kuhakikisha uaminifu wa uchaguzi.

  Pia amesema marais hao wamesisitiza kuwa kuchelewa kutolewa kwa matokeo ya uchaguzi kunaweza kuleta mashaka na kuvuruga amani na utulivu wa nchi hiyo. DRC ilifanya uchaguzi Desemba 30 mwaka jana na matokeo yalipangwa kutangazwa Januari 6.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako