• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Ukarabati wa reli kati ya Zambia na Malawi wakamilika

  (GMT+08:00) 2019-01-10 09:36:13

  Msemaji wa Shirika la Reli la Zambia amesema kazi ya ukarabati wa reli ya pamoja ya Zambia na Malawi, kwa upande wa Zambia imekamilika, huku ukarabati wa reli hiyo upande wa Malawi ukiendelea.

  Kazi ya usafiri kwenye reli ya Chipata-Shinji ilisimamishwa kwa muda mwezi uliopita kutokana na mvua kubwa iliyoathiri reli hiyo.

  Meneja mtendaji wa Mahusiano ya Umma wa shirika la Reli ya Zambia Bw. Sombe Ng'onga, amesema wakati ukarabati kwenye upande wa Malawi unaendelea, usafiri wa reli kati ya mji wa Chipata mashariki mwa Zambia kuelekea Bandari ya Nacala nchini Msumbiji utaanza kabla ya mwisho wa mwezi huu ukarabati utakapokamilika.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako