• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Kumekucha uchaguzi Yanga, Kampeni zaanza rasmi

  (GMT+08:00) 2019-01-10 10:38:58

  Wakati kipyenga cha kampeni za uchaguzi wa Yanga kikipulizwa kuashiria kuanza kwa kampeni za kugombea nafasi mbalimbali za uongozi katika Klabu ya Yanga ya jijini Dar es Salaam Tanzania, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi ya shirikisho la soka la Tanzania (TFF) Malangwe Mchungahela ametoa onyo kwa wanachama wa klabu hiyo wanaowatisha wagombea wanaotaka kufanya kampeni katika matawi yao.

  Mchungahela ameeleza kuwa, uchaguzi huo unatarajia kufanyika Januari 13 mwaka huu katika ukumbi wa bwalo la maofisa wa polisi Oysterbay jijini Dar es Salaam.

  Jumla ya wagombea 16 wanawania nafasi mbalimbali za uongozi, uchaguzi huo ni muhimu kuziba nafasi za wagombea waliojiuzulu kwa nyakati tofauti baada ya uchaguzi wa Juni 11 mwaka 2016.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako