• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Makamu rais wa China ahudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 40 tangu China na Marekani kuanzisha uhusiano wa kibalozi

    (GMT+08:00) 2019-01-10 19:02:54

    Makamu wa rais wa China Bw. Wang Qishan amehudhuria hafla ya kuadhimisha miaka 40 tangu China na Marekani kuanzisha uhusiano wa kibalozi iliyofanyika leo hapa Beijing.

    Akizungumza kwenye hafla hiyo, Bw. Wang amesema, baada ya miaka 40, uhusiano kati ya China na Marekani umeingia kwenye kipindi kipya, pande mbili zinapaswa kushikilia msingi wa uratibu, ushirikiano na utulivu, utakaonufaisha zaidi nchi hizo mbili na dunia nzima.

    Bw. Wang amesema, makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa China na Marekani yameonyesha mwelekeo wa kuendeleza zaidi uhusiano kati ya nchi hizo mbili, ambao una umuhimu mkubwa zaidi duniani.

    Pia amesisitiza kuwa, pande hizo mbili zinapaswa kufuata hali mpya, kutafuta na kupanua mambo yanayohusiana na maslahi ya pande mbili, na kuzidisha na kuhimiza ushirikiano, ili watu wa nchi hizo mbili waweze kunufaika zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako