• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Korea Kusini asema mazungumzo ya pili ya viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani yatafanyika hivi karibuni

  (GMT+08:00) 2019-01-10 19:04:05

  Rais Moon Jae-in wa Korea Kusini amesema mazungumzo ya pili kati ya Korea Kaskazini na Marekani yatafanyika hivi karibuni.

  Rais Moon Jae-in amesema, katika mwaka mmoja uliopita, kutokana na juhudi za pande mbalimbali, peninsula ya Korea ilielekea kwa amani, na mchakato wa amani ya peninsula hiyo utaendelea kuharakishwa, na kwamba China imechukua nafasi kubwa katika kuhimiza mazungumzo kuhusu peninsula hiyo.

  Rais Moon amesema, ziara ya kiongozi wa Korea Kaskazini Bw. Kim Jong-un nchini China hivi karibuni imeonesha kuwa mazungumzo ya pili kati ya Korea Kaskazini na Marekani yanakaribia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako