• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa ataka utulivu nchini DRC baada ya vurugu kutokea baada ya kutangazwa matokeo ya uchaguzi

  (GMT+08:00) 2019-01-10 19:25:15

  Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezitaka pande husika katika uchaguzi uliofanyika hivi karibuni nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kutofanya vurugu baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa.

  Taarifa iliyotolewa na Msemaji wa katibu mkuu huyo Stephane Dujarric imesema, Bw. Guterres ametaka mgogoro wowote unaosababishwa na matokeo ya uchaguzi huo unapaswa kusuluhishwa kwa kufuata njia sahihi kuendana na katiba ya DRC na sheria za uchaguzi.

  Uchaguzi mkuu ulifanyika Desemba 30 nchini DRC ambapo mgombea wa upinzani Felix Tshisekedi alitangazwa mshindi na Tume ya Uchaguzi nchini humo mapema leo kwa kupata kura zaidi ya milioni 7.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako