• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mazungumzo kuhusu suala la miundo kati ya China na Marekani yapata maendeleo

    (GMT+08:00) 2019-01-10 19:41:00

    Msemaji wa wizara ya biashara ya China Bw. Gao Feng leo hapa Beijing amesema, mazungumzo ya ngazi ya naibu mawaziri kati ya China na Marekani kuhusu suala la uchumi na biashara yameongeza muda, hii inaonyesha kuwa pande mbili zina msimamo wa makini na wazi, na mazungumzo kuhusu suala la miundo yamepata maendeleo.

    Bw. Gao Feng amesema, suala la miundo ni muhimu katika mazungumzo hayo, na pande hizo mbili zimepata maendeleo kuhusu suala hilo, zimeongeza maelewano, pia kuweka msingi kwa ajili ya kutatua mambo yanayofuatiliwa nazo.

    Pia amesema, ujumbe wa kila upande umebadiliana maoni kwa kufuata makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi hizo mbili, na katika kipindi kijacho, pande hizo zitaendelea kushirikiana na kuhimiza mazungumzo kwa mpango uliowekwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako