• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya: Safaricom yaanzisha huduma ya kuwezesha wateja kukopa pesa kupitia M-pesa

  (GMT+08:00) 2019-01-10 19:47:38
  Wateja wa huduma ya kutuma na kupokea pesa kwa simu maarufu kama M-Pesa nchini Kenya sasa wanaweza kununua bidhaa au kutuma pesa wakiwa hawana pesa katika akaunti zao za simu.

  Hii ni baada ya Safaricom kuzindua mpango wa Fuliza kwa watumiaji wote wa M-Pesa nchini.

  Safaricom iliamua kuanzisha mpango huo baada ya kuufanyia majaribio Novemba mwaka 2018.

  Watumiaji wa M-Pesa nchini Kenya ni 24.2 milioni na wanatarajiwa kunufaika na mpango huo mypa.

  Kwa kutumia Fuliza, wateja watakuwa na uwezo wa kutumia hadi Sh50, 000 kulingana na kiwango wanachohitaji.

  Kampuni hiyo inashirikiana na Benki ya KCB na CBA. Mteja akichukua, atalipa kwa riba ya asilimia 0.5 kwa siku.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako