• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania: TRA imeanzisha utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara

  (GMT+08:00) 2019-01-10 19:47:59
  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), imeanzisha utaratibu wa kukutana na wafanyabiashara ili kusikiliza kero na malalamiko yao kila siku ya Alhamisi.

  Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa kodi wa TRA, Richard Kayombo amesema siku hiyo itakuwa maalum kwa mameneja wa mamlaka hiyo wa mikoa na wilaya kote nchini kusikiliza na kutatua kero za walipakodi.

  Aidha, alisema TRA imeanzisha kituo cha ushauri kwa walipakodi kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambacho kipo katika jengo la NHC Samora, lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na kuwa karibu na walipakodi na vituo kama hivyo vitafunguliwa kote nchini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako