• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Hospitali ya kijeshi ya Rwanda kuwaandaa wapasuaji wa kurekebisha sura

  (GMT+08:00) 2019-01-11 08:54:27

  Hospitali ya kijeshi ya Rwanda imesema itafanya kazi kama kituo cha mafunzo ya upasuaji wa kurekebisha sura kwa ajili ya Chuo cha Upasuaji cha Mashariki, Kati na Kusini mwa Afrika COSECSA, kitakachosaidia kuwaandaa wapasuaji wengi zaidi wa kurekebisha sura nchini Rwanda ili kuziba pengo la ukosefu wa wataalamu hao.

  Mpango huo wa mafunzo unatarajiwa kuongeza idadi ya wapasuaji wa kurekebisha sura nchini Rwanda kutoka wawili wa sasa.

  Mtaalamu wa pasuaji za kurekebisha sura wa hospitali hiyo Bw. Charles Furaha amesema mpango huo utasaidia kuwaandaa wapasuaji wanaoweza kukidhi mahitaji ya juu ya wagonjwa wanaotafuta kurekebisha sura zao, na kwamba hivi sasa wagonjwa nchini Rwanda wanahitaji kusubiri kwa miaka minne kabla ya kufanyika pasuaji za aina hiyo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako