• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mwendo wa kasi kupita kiasi watajwa kuwa chanzo cha ajali ya treni Afrika Kusini

  (GMT+08:00) 2019-01-11 08:54:44

  Uchunguzi wa awali uliofanywa na Mamlaka ya usalama wa reli ya Afrika Kusini unaonesha kuwa mwendo wa kasi kupita kiasi umetajwa kuwa ni chanzo cha ajali ya kugongana kwa treni mbili iliyotokea mjini Pretoria na kusababisha vifo vya watu watatu, na wengine zaidi ya 600 kujeruhiwa.

  Ajali hiyo ilitokea Jumanne wakati treni moja iliyokuwa ikielekea kituo cha Pretoria iligonga nyuma ya treni nyingine iliyokuwa imesimama kwenye kituo cha Mountain View.

  Msemaji wa kampuni ya treni nyepesi za mijini ya Afrika Kusini Bibi Lilian Mofokeng amesema treni zinazosafiri kati ya Pretoria na Mabopane zinadhibitiwa na madereva, na zinatakiwa kusafiri kwa mwendo kasi wa kilomita 30 kwa saa, na kuongeza kuwa mwendo wa kasi huenda ni chanzo cha ajali ya Jumanne lakini kasi yake halisi itathibitishwa baadaye.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako