• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Wanajeshi watatu wajeruhiwa baada ya watu wenye silaha kuvamia shule Cameroon

  (GMT+08:00) 2019-01-11 09:04:37

  Wanajeshi watatu wamejeruhiwa baada ya watu wenye silaha kufanya shambulizi, katika eneo la Kumba, lililoko katika sehemu ya kusini magharibi mwa Cameroon wanakotumia lugha ya kiingereza.

  Taarifa iliyotolewa na jeshi la Cameroon inasema wanajeshi hao wamejeruhiwa wakati kundi la wafarakanishaji linavamia shule moja ya sekondari, na kikosi cha pamoja cha jeshi na polisi kilikwenda kwenye eneo hilo ili kutuliza hali. Baadhi ya wafarakanishaji walijeruhiwa kwenye tukio hilo.

  Kwenye hotuba ya mwaka mpya Rais Paul Biya wa Cameroon alionya kuwa wafarakanishaji wenye silaha watashughulikiwa kama hatawataweka chini silaha zao na kufuata njia sahihi. Jumuiya ya wanadiplomsia nchini Cameroon imemtaka Rais Biya kuondoa mgogoro kwa njia ya mazungumzo shirikishi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako