• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Serikali ya Yemen yalaani shambulizi la drone lililofanywa na kundi la Houthi

  (GMT+08:00) 2019-01-11 09:05:00

  Serikali ya Yemen inayoungwa mkono na Saudi Arabia imelaani vikali shambulizi la ndege isiyo na rubani lililofanywa na waasi wa Houthi wanaoungwa mkono na Iran, dhidi ya wanajeshi waliokuwa kwenye gwaride katika jimbo la kusini la Lahj.

  Taarifa iliyotolewa na shirika la habari la nchi hiyo Saba inasema shambulizi hilo ni uchokozi ulio wazi dhidi ya jumuiya ya kimataifa. Serikali imeitaka jumuiya ya kimataifa kuwa na msimamo mkali dhidi ya waasi wa Houthi ambao wanakiuka mara kwa mara makubaliano ya kusimamisha vita, na kukataa kufuata makubaliano ya Sweden.

  Akizungumzia mazungumzo hayo Waziri wa mambo ya nje wa Yemen Bw. Khaled Al Yaman amesema hakuna maendeleo yaliyopatikana tangu makubaliano hayo yasainiwe. Amesema mwezi mmoja tangu makubaliano hayo yasainiwe waasi wamekuwa wakikiuka makubaliano na hawajaondoka kwenye bandari.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako