• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Umoja wa Afrika wahimiza DRC kuimarisha demokrasia na kudumisha amani baada ya matokeo ya uchaguzi kutangazwa

  (GMT+08:00) 2019-01-11 09:13:53

  Mwenyekiti wa kamati ya Umoja wa Afrika Bw. Moussa Mahamat amesisitiza kuwa pande zote husika za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo DRC zinapaswa kuimarisha demokrasia na kulinda amani, baada ya matokeo ya awali ya uchaguzi wa rais kutangazwa.

  Katika taarifa ya Umoja wa Afrika, Mahamat ametambua matokeo ya awali yaliyotangazwa na tume ya uchaguzi. Amewapongeza wananchi, wanasiasa, jamii na serikali ya DRC kwa kupata mafanikio katika uchaguzi huo, ambao umeuridhisha ujumbe wa waangalizi wa uchaguzi wa Umoja wa Afrika uliongozwa na rais Dioncounda Traore.

  Msemaji wa katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric jana amesema Umoja wa Mataifa unafuatilia kwa karibu hali ya DRC kutokana na mgogoro wa matokeo ya chaguzi, hali ambayo ingesababisha ukosefu wa utulivu nchini humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako